Saturday, March 31, 2012
Walipewa cheti cha PF90kwa ajili ya kupeleka kwenye ofisi za BIMA kwa ajili ya ukarabati wa magari yote yalio pata ajali (yaani gari langu na la kwao )
mimi nilikua nikifanya kazi katika kampuni moja ilioitwa ISI-H engenearing company limited, kwa kifupi ilijulikana kama (I E C L) nilikua kama msaidizi kwa lugha ya kigeni ni secretary wa kampuni ile iliokua ikifanya kazi maeneo ya nduli kama kilometa tano kabla kufika kwenye kiwanja cha ndege cha nduli.
kampuni ile ilikua ikitengeneza barabara ile iliotoka iringa mjini hadi mkoa wa dodoma kwa kiwango cha lami. ama kweli niliamini msemo wa wahenga usemao "fimbo ilio mkononi, ndio iuayo nyoka". kuna msaidizi wangu kazini alipoona sirudi kazini kwa muda tuliopewa kwenda kupata mlo wa mchana, alijaribu kudadisi ni nini kimetokea kwangu mpaka muda ule sijarudi kazini na alipo gundua niliondoka na gari na kukutana na mwanamke yule niliemsaidia kwa kuzidiwa kuzimia na kumpeleka hospitali;
msaidizi wangu alie julikana kwa jina la poteza baki alienda mpaka kwa bosi na kumueleza kua mimi niliondoka na mwanamke na kwenda kula raha kwenye mahoteli ya iringa mjini. bosi aliposikia hivyo alijaribu kushika simu yake ya mkononi na kubofya namba zangu za simu yangu na alipojaribu kupiga haikua hewani namaanisha ilikua haipatikani kwa sababu simu yangu ilisagwa chini pindi tulipopata ajali ile na ikaharibika kabisa. bosi alikasirika na kuandika barua ya kufukuzwa kazi na kumuachia poteza ili aje anipe nikirudi kazini.
haikupita muda mrefu sana nilitafuta kibanda cha kupigia simu na kumpigia bosi kwa kua namba za bosi nilizifahamu haikunipa shida sana. nilipompigia simu bosi na kumueleza yote yaliotokea, bosi hakunielewa kabisa na kwakua bosi alimuamini sana poteza ilibidi ampe alama mia moja kwa mia moja kwa kumueleza kilichotokea kwangu ingawa ilikua si kweli. .................
USIKOSE MUENDELEZO WA STORY HII WIKI IJAYO....................
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment