Saturday, March 10, 2012

JE WAIJUA NDOTO YA BARNABA

BARNABA
Toka nyumba ya kukuza vipaji ya THT, Barnaba alikuwa na kifua cha kuweka wazi kuwa moja ya mikakati yake mikubwa ilikuwa ni kugonga kazi moja na bishoo mkongoman  Fally Ipupa.
Lakini maneno ya Barnaba hayakuwa ya bure tu kwani yalitokana na MkongoMan huyo kumfagilia Barnaba kwenye ukurasa wake wa Twiter kuwa anafurahishwa na kazi za bwana mdogo huyo toka Bongo na kuahidi kuwa ipo siku atafanya nae kazi.
Hapa ananukuliwa Fally toka ukurasa wake wa Twitter;
"Nimeridhishwa na kiwango cha mwanamuziki kutoka Tanzania Barnaba na nina nia ya kufanya nae kazi atakapokuwa tayari"ni baadhi ya maneno yalivyosomeka kwenye ukurasa wa Twiter wa mwanamuziki huyo kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
KILICHOJIRI WAKATI WA ZIARA YA FALLY IPUPA MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA
Taarifa rasmi ni kwamba kolabo hiyo inafanywa wiki hii na itarekodiwa katika studio za THT Dar es salaam.
Barnaba mwenyewe anaweka wazi kuwa litakuwa ni songi la mahaba litakaloitwa 'TUACHANE KWA WEMA',
Akiendelea kufunguka, Barnaba anasema kolabo hilo amelipata free kabisa bila kumlipa Fally hata shilingi 100, na hii ni kutokana na bishoo huyo wa kikongo kuzimikia kazi za Barnaba tangu muda mrefu.
Hii kolabo inafanyika miezi mitatu baada ya Fally Ipupa kukubali kupitia twitter kwamba anamjua na anakubali uwezo wa BARNABA na yuko tayari kufanya nae kolabo.

No comments:

Post a Comment