Tuesday, March 27, 2012
BONGO BILA SKENDO
Naomba niongele skendo za wasanii bongo kwa uchungu na hisia ambazo naziona katika jicho langu la tatu. si mara moja au mara mbili kumekua kukitokea skendo za wasanii wa bongo kuchafuana wenyewe kwa wenyewe,wasanii kwa wahandishi wa habari bega kwa bega kufuatiliana. hivi ni vyema kwa wasanii kurukaruka kama kima na kufanya mambo ya ajabu na kuweka maswali kwa vichwa vya watu chungu mzima. hii inatokana na nini mimi nadhani ni ukosefu wa maadili kwa wasanii wa sasa.
hivi ni kitu gani kinacho wafanya muache kufanya mambo ya kazi zenu na kufanya uzinzi hadharani, starehe zilizopindukia.
enyi wasanii acheni hayo mambo mna dhalilisha heshima ya nchi tanzania na pia hamjengi picha nzuri kwa jamii inayo wazunguka na kuwasikiliza kama wasanii.
wasanii badilikeni ili muwe fundisho zaidi kwa jamii inayo wazunguka na hii itafanya muheshumike na muonekane watu ambao wana mchango mkubwa katika jamii....BONGO BILA SKENDO INAWEZEKANA..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment