bendera yetu tanzania |
Mfumo wa vyama vingi ni hali ya kuwa na chama zaidi ya kimoja,katika nchi moja.Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa,ili kuleta maendeleo ya nchi,upinzani wa kisiasa sio uadui kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani,kuwa na vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii huska.
Tanzania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa uliorejeshwa katika katiba ya Tanzania mwaka 1992.
Chama tawala ni
Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama tawala nchini Tanzania. CCM ilizaliwa 5 Februari, 1977 baada ya kuungana kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala cha Zanzibar wakati huo. Chama cha Mapinduzi kilikuwa kikiongozwa na Mwalimu Nyerere na Afro-Shiraz Party kilikuwa chini ya Amaan Karume.
Kwa miaka mingi CCM ilikuwa ikifuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Itikadi hii ilipewa nguvu za kisera mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la Arusha. Kutokana na azimio hilo uchumi uliwekwa mikononi mwa umma. Itikadi hii pia ilisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja hasa katika vijiji vya Ujamaa.
Tanganyika African National Union (TANU) kilikuwa chama kilichotawala Tanganyika na Tanzania hadi muungano wa chama hiki na Chama cha Afro-Shirazi cha Zanzibar ulipounda Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977.
TANU ilianzishwa Julai 7, 1954 kutokana na Tanganyika African Association (TAA). TAA ilikuwa na mwelekeo wa kitamaduni zaidi ya siasa. Mwenyekiti wa kwanza wa TANU alikuwa Julius Kambarage Nyerere.
TANU ilishinda kila uchaguzi chini ya utawala wa kikoloni ikawa chama cha kuongoza Tanzania hadi ilipopata uhuru wake mwaka 1961. Katiba ya Taifa ya mwaka 1962 ilifanya TANU kuwa chama cha pekee nchini ikifuata mfano wa nchi za kijamaa zenye muundo wa siasa ya chama kimoja.
Afro-Shirazi Party (kifupisho: ASP) ilikuwa chama cha siasa kisiwani kwa Zanzibar. Ilianzishwa wakati vyama viwili vingine, yaani Shiraz Party ya Waajemi na Afro Party ya Waafrika, vilipoungana. Uanzishaji wa chama hilo ukasababisha uondoaji wa Waarabu kutoka utawala wa Zanzibar katika mapinduzi ya mwaka wa 1964. Mwaka wa 1977, ASP ilijiunga na TANU kuwa Chama cha Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment