JOSHUA NASARI PHYLOSOPHY KABLA NA BAADA YA USHINDI WA KISHINDO
Tumeanza na Mungu, tutamaliza na Mungu – Joshua Nasari
“Cha kwanza kabisa namshukuru sana Mungu ambaye alinipa maono ya kuwa mbunge wa Arumeru mashariki, nimekuwa nikiyasema kwa muda mrefu watu walifikiri natania, lakini vilevile nikishukuru chama changu cha CHADEMA ambacho kilinipa ridhaa ya kusimama kuwakilisha kwenye uchaguzi mdogo wa Arumeru mashariki, kwakweli niwashukuru sana watu wa Arumeru mashariki ambao hawakujali umri wangu, hawakujali uwezo wangu kifedha, hawakujali historia ya familia yangu katika siasa, hawakujali kila mapungufu ambayo nilikuwa nayo, lakini wakaamua kunichagua…..napenda niseme na kama nilivyosema tangu mwanzo kwamba tumeanza na Mungu na tutamaliza na Mungu na siyo kwenye kupata kura peke yake, tutaendelea kumtumikia Mungu na kumuweka Mungu mbele, tutamtanguliza yeye na tutaongozwa na yeye siku zote”
Haya ni maneno ya mbunge wa CHADEMA mtumishi wa Mungu, Joshua Nasari (26) aliyeshinda Jimbo la Arumeru mashariki kwa kura 32972 ambazo ni sawa na asilimia 54 na kufuatiwa na mgombea wa chama cha mapinduzi, Sioi Sumari aliyepata kura 26,757 sawa na asilimia 42.
No comments:
Post a Comment