Friday, December 9, 2011

HONGERA TANZANIA LAKINI???

Na isihaka myanza
  Bidii ya viongozi wetu kuanzia awamu ya kwanza iliyo shikiriwa na hayati baba wa taifa mh mwalimu julius kambarage nyerere mpaka sasa yupo mzee wa nguvu mpya na kasi mpya mh jakaya mrisho kikwete, ni mabadiliko mengi yamefanyika ya kimaendeleo kwa mfano shule kuongezeka na barabara kifupi ni huduma muhimu zinaonekana kupamba moto si kama enzi zile na sasa. kwa hali hii sina budi kusema hongera tanzania kwa kufikisha miaka hamsini tangu uhuru mpaka sasa kwa kupiga hatua kimaendeleo. hongera sana sana.......





    LAKINI? hebu tujiulize watanzania tumepata shule nzuri za kata, hospitali zenye majengo mazuri, barabara nz
uri. lakini zinatumika vile inavyopaswa? shule zina maabara na vitabu vya kutosha? hospitali zina dawa na wahudumu wazuri, walimu je? nao wanapata haki zao za msingi? serikali iko wapi kutetea haki za msingi za wafanyakazi? hii ndio tanzania ya sasa. mafisadi hawaishi viongozi wanafanya vitu kimaslahi yao. miaka hamsini ya uhuru tumefanya nini??? sehemu hii ina viulizo vingi kwasababu naongea kwa uchungu na kuonyesha msisitizo mtanisamehe kama ninakosea lakini inauma kwanini tanzania hii haishi siasa za uongo viongozi wanaongea vitu wasivyo tekeleza tunakwenda wapi tanzania?........

No comments:

Post a Comment