Saturday, February 25, 2012

MTUNZI:ISIHAKA SALUM MYANZA
 E MAIL: isihakamyanza@gmail.com
MOBILE NO: 0766937781 or 0654284877
 
                    SEHEMU YA KWANZA
 
Ilikua ni siku ya jumatano ambapo nilimuona mwanamke mmoja ambae sikuweza kumtambua jina kwa haraka. Alikua akitembea katika barabara moja iliokua ya vumbi iliyoitwa DODOMA ROAD iliyopo huko mkoani Iringa. Mwanamke huyo aliekua anaonekana amechoka sana na mwenye matatizo makubwa lakini pia alionekana mwenye majonzi usoni mwake ukimtazama.

Yalikua ni majira ya saa sita mchana ambapo jua lilikua likichoma sana huku mimea ikinyon’gonyea mithili ya mbwa alie tishiwa kupigwa akaogopa na kukalia mkia wake. Wafanyakazi wa serikali na watu binafsi walikua wakijiandaa kwenda kula chakula cha mchana katika mahoteli, migahawa na wengine kwenda majumbani mwao ili kupata mlo huo wa mchana. Wengine pia bila kujali wakiendelea kufanya kazi nzito bila kujali huo ulikua ni mda wa kupata chakula cha mchana, si kwamba walikua hawana pesa ya kununulia chakula? La hasha! Walijali sana kazi kuliko kula, lakini walipo jihisi njaa ndipo nao walipojipatia chakula kukidhi haja ya matumbo yao.

Mimi nilikua kwenye gari dogo aina ya Suzuki nilikua nikielekea kwa mama ntilie tulie mzoea kwa jina la mama sheteshete, tulifupisha jina lake na kumuita mama shete. Nilikua naenda kwa mama shete ili nami nipate mlo wa mchana ili nikidhi haja ya tumbo langu. Hapo ndipo nilimuona mwanamke ambae alikua amechoka sana na alikua katika majonzi. Nilimuonea huruma, kwavile nilikua kwenye gari, niliegesha gari langu pembeni ya barabara ile ambayo ilikua ni yenye vumbi lenye rangi nyekundu. Nilishuka ndani ya gari na kumtazama mwanamke yule  masikini! Alikua amevaa kanga ambayo imechanika na kutoboka  utadhani imeliwa na panya na miguuni mwake alikua amevaa kandambili ambazo zilikua tofauti (dongea) pia zilikua zime chafuka pamoja na miguu yake kwa dongo na vumbi jekundu mithili ya mtu alietoka kuchimba ama kulima shamba angali bado kiangazi. Nilitamani nilie lakini nilibaki nimekodoa macho mithili ya mjusi aliebanwa na mlango.

Ghafla mwanamke yule akiyumba kama mlevi aliekunywa pombe nyingi. Alianguka puu!! Mwanamke yule kama kiroba cha unga ama kifurushi cha nguo. Nilimkimbilia na nilipofika karibu yake nilikuta amepoteza fahamu. Hapo akili yangu haikuwaza tena kwenda kula kwa mama shete. Nilifikiri ni jinsi gani naweza kumsaidia mwanamke yule. Nilimbeba na kumpeleka kwenye gari langu na kuwasha moja kwa moja hadi hospitali iliokua mbali na eneo hilo. Nilienda mwendo kasi kwani niliogopa asije akafa kwani alikua akitoka jasho mithili ya mtualie mwagiwa maji usoni. Nilikua nikimpeleka katika hospitali ya mkoa wa iringa iliopo mjini iringa kwani tulipotoka kulikua hakuna hospitali wala zahanati karibu.

Tulipita kama kilometa tano ndipo tuliikuta barabara ya lami ambayo ilikua karibu na kiwanja cha ndege cha mkoa wa iringa kilichoitwa nduli.

Nilimwangalia mwanamke yule usoni, alionekana ni mtu aliezidiwa sana na jasho lilizidi kumtoka usoni mwake. Nilijawa na hofu sana nikifikiri endapo atafariki nitafanya nini? Nilijiuliza maswali mengi ambayo sikuweza kupata majibu mapema kwa hofu nilio kuanayo. Yule mwanamke ambae sikumfahamu jina alizidi kutokwa na jasho hadi sehemu nilio muweka ikalowana tepe tepe. Nilichukua kitambaa changu kidogo (leso) huku nikishika usukani kwa mkono mmoja na mkono mwengine nikijaribu kumfuta jasho mwanamke yule, bila mafanikio jasho liliendelea kumtoka kwa kasi.

Nilitaka kukata tamaa kwani nilipo muangalia mgonjwa alikua bado hanipi matumaini kama anaweza kupona lakini nilipiga moyo konde na kujipa matumaini ingawa ni matumaini hafifu. Niliongeza mwendo kwa kuamini nikifanya hivyo nitawahi kufika katika hospitali hiyo ya mkoa.

Huku nikiongeza mwendo katika  gari kwa mkono mmoja nilishika usukani na kujaribu kufungua madirisha ya gari hilo kwa mkono mwingine. Baada ya muda takribani dakika tatu mpaka tano baada ya kufungua dirisha lililopo karibu na mgonjwa, nilimuona mgonjwa akijaribu kufumbua macho kwa mbali ingawa bado hali yake haikua nzuri.

Lakini mimi niliona akipata ahueni kwa vile alikua hawezi hata kufumbua macho. Nadhani ule upepo uliokua ukiingia ndani ya gari kwa sababu ya mwendo kasi ulimfanya mgonjwa yule apate ahueni.

Nilijaribu kumuita kwa kusema Halo! Halo! Huku huku nikimtikisa kwa mkono mmoja, lakini hakuweza kuongea wala kuitika, macho yake yali fumba na kufumbua kama mtu alietaka kusinzia angali hataki usingizi.

Nilizidi kwenda mwendo kasi ndipo tulipofika sehemu moja iitwayo mgongo, sehemu hii ina kona kali sana ambazo hutakiwi kwenda mwendo kasi. Nilipunguza mwendo ingawa ni kidogo. Ghafla lilitokea lori ambalo sikujua mapema kwamba limebeba nini. Lori hilo lilitokea mbele yetu katika kona hizo za mgongo na lilikua limewasha taa zote angali ni mchana na lilikua likipiga honi mara kwa mara likionyesha ishara ya hatari na lilikua likiyumba barabara nzima. Lori hili lilipoteza mwelekeo nami sikuweza kulikwepa kwani barabara ilikua ni ndogo,upande mmoja wa barabara ni mlima na upande mwine ni bonde kubwa.
..........................itaendelea

Thursday, February 9, 2012

SITAKI KUINGIA KILI MUSIC AWARDS

mr misifa (dully sykes)
Baada tu ya kutangazwa kw anominees wa tuzo za KILI TANZANIA MUSIC AWARDS msanii kutoka ilala mzee wa bongo fleva Dully Sykes amekuja juu na kulaumu uongozi kwa kumuweka katika kinyang'anyiro cha tuzo za kili. nilishawaambia sitaki kuwepo tena katika tuzo zao, tangu mwaka juzi wakati wa shikide, lakini nashangaa kuona wanaendelea kuniweka tu, kwani wananiona mimi ndio masanii pekee, wakatu ule wa hits kama nyambizi, Hi na zinginezo mbona hawakunipa tuzo? au walidhani mi ni msanii ambae ningeishia kati tu, lakini baada ya kuona nipo na naendelea kuwepo ndio wanajifanya kunitambua..ni mesema sitaki.

baada ya dully kuongea hayo, tulipata nafasi ya kuongea na mzee Luhala kutoka BASATA na e alisema haya.
" kama msanii ameamua kujitoa basi aandika barua BASATA ya kujitoa lakini sio kwa maneno tu"
'