Saturday, March 10, 2012

 
SEHEMU YA PILI
Lori lile lilituvaa na lenyewe likakita katika ukuta wa mlima ule na gari letu liliingia bondeni na kupinduka na kuvunjika vioo vyote. Sikuumia sana, nilichubuka kwenye mikono yangu na usoni kidogo kwa vioo vile vilivyo vunjika.

Masikini mwanamke yule alikua amechubuka kiasi na alikua amezidiwa kabisa kiasi cha kutoa povu mdomoni. Nilimuonea huruma huku nikijilaumu mwenyewe. Kwani nilihisi mimi ndie nilie msababishia yote hayo. Nilidhani amefariki kwani alitoa povu jingi sana mdomoni na puani mwake. Mimi nilikua mwenye fahamu na nilijitahidi kujinasua kwenye gari hili lililo pinduka ili nikitoka nimtoe na mwenzangu lakini ilishindikana kabisa kwani gari lile lilikua lime bonyea sana.

Bila kutegemea nilisikia sauti ya gari lililopiga kelele ya kuashiria kuna hatari imetokea. Lilikua ni gari la hospitali  kuu ya iringa ilio julikana kwa jina la “government hospital” lilikua na daktari mmoja na wauguzi wawili vilevile liliongozana na gari la polisi aina ya land rover lenye namba PT 220 lililokua na polisi sita.

Polisi wale walijitahidi kutung’oa kwenye adha ile na kutuweka kwenye gari maalum la wagonjwa na kutupeleka katika hospitali kuu ya mkoa wa iringa. Polisi wale watatu kati yao walikua ni polisi wa usalama barabarani na wengine watatu walikua wakitoka katika kikosi cha kutuliza ghasia (FFU).

Tulifikishwa katika hospitali ya mkoa wa iringa ilikua ni majira ya saa saba na nusu mchana. Tulitibiwa lakini mimi nilipata ahuweni haraka kwasababu nilikua sina majeraha mengi. Baada ya siku mbili niliruhusiwa kwenda nyumbani, mwenzangu alikua bado yupo kwenye hali mbaya na aliwekewa mipira ya kuongezewa maji kwenye mishipa yake ya mikono. Nilimuuliza daktari kua ni kiasi gani cha fedha kimetumika kututibu na ni nini kinahitajika kwa wakati huu ili niweze kulipa kila kitu. Kwa wewe unahitaji kulipa elfu kumi na mbili za matibabu yote tulio kutibia na mwenzako bado mpira mmoja wa maji na dawa ambazo atakunywa baada ya kumaliza mpira huo wa maji ambapo gharama ya vitu vyote hivyo ni shilingi elfu thelathini na tano pesa taslimu za kitanzania “alisema daktari ambae alifahamika kwa “doctor huruma Jordan”. Bila kuchelewa nilitoa pesa katika mfuko wa suruali yangu iliokua imechanika kidogo miguuni na vioo vilivyopasuka baada ya ajali ile na kumkabidhi pesa doctor huruma  Nilimkabidhi kiasi alicho kisema na kumsisitiza amuangalie mgonjwa wangu vizuri mpaka atakapo pata ahueni na kupona kabisa. Dactari huruma alinihakikishia kwa maneno matamu kua nisiwe na hofu mgonjwa atapona na atarudi katika hali yake ya kawaida huku akinishika bega na kucheka na kutabasamu kwa matumaini na akaondoka kwa madaha huku koti lake lenye rangi nyeupe lililong’ara likipepea kwa upepo mwanana uliopiga katika eneo hilo la hospitali.

Katika lori lile lililotugonga kulikuwepo na dereva aliejulikana kwa jina la magia na utingo wa mizigo alieitwa mabavu. Walikua wamebeba matunda aina ya mananasi ambayo walitokanayo makambako katika mashamba ya mfanyabiashara binafsi wakipeleka mzigo huo huko dodoma wilayani mpwapwa.

Wenyewe hawakuumia sana kwani gari lao lilipasuka taa za mbele tu kwa kukita kwenye ukuta ule wa mlima mrefu uliopo kwenye eneo hilo lilipo tokkea ajali hiyo. Dereva na utingo wa gari kubwa walipelekwa lumande kwa kutozingatia sheria za barabarani. Walijitetea kwa kusema kwamba gari lile lilipoteza uelekeo kwa kukosa breki, hapo tulikua hatuna jinsi ya kujitoa kwani tulikua kwenye kona kali na gari letu lilikua likienda mwendo kasi hapo tulijitoa muhanga na ajali ilipotokea ilikua ni bahati mbaya. “alisema dereva wa lori lile”. Walisamehewa kwa kuwekwa lumande siku tatu na kutolewa na kupewa cheti cha PF90 kwa ajili ya ukarabati wa magari yote yaliopata ajali..   USIKOSE MUENDELEZO WA THIS IS MY PAGE........
NEXT WEEK...

No comments:

Post a Comment