Monday, April 16, 2012

KILIMANJARO MUSIC AWARDS YATIKISA ILA KWA MAJONZI

  Ni tamasha kubwa ambalo hufanywa kila mwaka kwa kuwapa tunzo wasanii wanaofanya vizuri katika kazi zao na tunzo maalum kwa wasanii ambao walionekana kutoa mchango mkubwa katika muziki wa tanzania. tamasha lilikua ni kubwa la aina yake lilionekana kujaa kwa watu wasanii nao walionekana kuitikia wito wakongwe kwa wachanga.
    


   Lakini tamasha hili liligubikwa na majonzi pindi pale baadhi ya wasanii walipo onyesha kumkumbuka msanii mahiri kwa kutunga na kuigiza filamu na sio katika filamu tu hata katika muziki STEVEN CHARLES KANUMBA. mungu amrehemu. majonzi haya au msiba huu ulionekana kumgusa sana msanii BARNABA pia ilikua ni furaha kwake kwani pindi msanii wa filamu

baba steve
 kanumba alipo fariki ndipo siku hiyo alipo pata mtoto aliempa jina la steve kutokana na msiba huo mkubwa. lakini majonzi hayo ya msanii barnaba yalizimwa baada ya kupata tunzo ya mwimbaji bora wa mwaka.hongera barnaba kwa tunzo na mtoto...

Tuesday, April 10, 2012

NINI KILICHOMUUA STEVEN CHARLES KANUMBA?

jeneza lililo beba mwili wa marehemu kanumba

 
Msanii nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitaalamu kama BRAIN CONCUSSION, taarifa za kitabibu zimeeleza.

Taarifa hizo za ndani, zimepatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa hospitali ya taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehem, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa.Mmoja wa madaktari hao ambae aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya masaa mawili.

"tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu Brain Concussion" alisema. Kanumba alipata mtikisko huo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) "kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehem ya nyuma ua ubongo (cerebram), huua kwa haraka" alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma husababusha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.

"Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji unafeli na ndio maana tumekuta kucha za kanumba zikiwa na rangi ya blue, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ni dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji"

"Mtu aliepata mtikisko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.

Daktari mwingine alieshiriki katika uchunguzi huo ambae pia aliomba jina lake lisitahwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji. Alisema sehemu ya maini na maji maji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo

Saturday, April 7, 2012

JE WAJUA MAJINA YA WAJUMBE WA TUME YA KATIBA YA NCHI (TANZANIA)?



 Ni mh dr: rais jakaya mrisho kikwete akitangaza mabadiliko ya tume ya uundwaji wa katiba mpya ikulu jijini dar es salaam.

ni lazima tujue hatima ya katiba mpya sisi watanzania


TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
(Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83,Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7)
______________________________



ni hatua ya mwanzo katika mchakato wa kuunda katiba mpya
UONGOZI WA JUU

1. Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA - Mwenyekiti
2. Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino RAMADHANI -  Makamu Mwenyekiti

WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - BARA

1. Prof. Mwesiga L. BAREGU

2. Nd. Riziki Shahari  MNGWALI

3. Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI

4. Nd. Richard Shadrack LYIMO

5. Nd. John J. NKOLO

6. Alhaj Said EL- MAAMRY

7. Nd. Jesca Sydney MKUCHU

8. Prof. Palamagamba J. KABUDI

9. Nd. Humphrey POLEPOLE

10. Nd. Yahya MSULWA

11. Nd. Esther P. MKWIZU

12. Nd. Maria Malingumu KASHONDA

13. Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)

14. Nd. Mwantumu Jasmine MALALE

15. Nd. Joseph  BUTIKU 
WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - ZANZIBAR

1. Dkt. Salim Ahmed SALIM

2. Nd. Fatma Said ALI

3. Nd. Omar Sheha MUSSA

4. Mhe. Raya Suleiman HAMAD

5. Nd. Awadh Ali SAID

6. Nd. Ussi Khamis HAJI

7. Nd. Salma MAOULIDI

8. Nd. Nassor Khamis MOHAMMED

9. Nd. Simai Mohamed SAID

10. Nd. Muhammed Yussuf MSHAMBA

11. Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN

12. Nd. Suleiman Omar ALI

13. Nd. Salama Kombo AHMED

14. Nd. Abubakar Mohammed ALI

15. Nd. Ally Abdullah Ally SALEH


UONGOZI WA SEKRETARIETI

1. Nd. Assaa Ahmad RASHID -  Katibu
2. Nd. Casmir Sumba  KYUKI -  Naibu Katibu 

TUTAMKUMBUKA MILELE STEVEN KANUMBA

MAREHEMU STEVEN KANUMBA




 Ni miaka ishirini na nane hivi sasa tangu kuzaliwa kwa nguli wa filamu tanzania (STEVEN CHALSE KANUMBA) imepita tangu mnamo mwaka 1984-2012. tarehe saba mnamo majira ya saa nane usiku ndipo yalimkuta mauti muigizaji steven kanumba.




ENZI ZA UHAI WAKE (STEVEN KANUMBA)



    Ni jambo la kusikitisha sana kwani ni kifo cha ghafla sana kutokea kwa msanii nyota kama huyu, pia ni jambo la kushtusha sana kwani ni kijana mdogo ambae anategemewa na familia yake. si familia tu pia taifa zima linamtegemea kwa kiwango kikubwa sana kwani ni muelimishaji jamii mzuri pia ni mmoja wa vijana ambao huingiza kipato kikubwa katika uchumi wa nchi yetu. 





ELIZABETH MICHAEL (LULU)




     KWA MUJIBU WA MDOGO WA MAREHEMU STEVE KANUMBA, ALISEMA KUWA ELIZABETH MICHAEL  MAARUFU KAMA LULU ALIKUJA NYUMBANI KUKAWA NA KAUGOMVI  AMBAPO WAKAINGIA CHUMBANI WAKIWA HUKO BAADA YA MUDA,LULU ALITOKA NA KUMUITA YEYE  KUMUAMBIA KANUMBA KAANGUKA, YE ALIPOENDA AKAMKUTA KAANGUKA NDIO AKAENDA MUITA DAKTARI WA KANUMBA AMBAPO ALIPORUDI HAKUMKUTA LULU, LAKINI  HADI TUNAVYOONGEA LULU YUKO POLISI OSTERBAY KWA AJILI YA MAHOJIANO NA POLISI, NA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA MUCHUARI MUHIMBILI. 
   
   BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA , KAMWE HATUTO MSAHAU STEVEN KANUMBA KWA KAZI YAKE NA UCHESHI WAKE MUNGU AMREHEMU NA AMUWEKE MAHALI PEMA PEPONI AMEN.........

Wednesday, April 4, 2012

JOSHUA NASARI PHYLOSOPHY KABLA NA BAADA YA USHINDI WA KISHINDO

Tumeanza na Mungu, tutamaliza na Mungu – Joshua Nasari

“Cha kwanza kabisa namshukuru sana Mungu ambaye alinipa maono ya kuwa mbunge wa Arumeru mashariki, nimekuwa nikiyasema kwa muda mrefu watu walifikiri natania, lakini vilevile nikishukuru chama changu cha CHADEMA ambacho kilinipa ridhaa ya kusimama kuwakilisha kwenye uchaguzi mdogo wa Arumeru mashariki, kwakweli niwashukuru sana watu wa Arumeru mashariki ambao hawakujali umri wangu, hawakujali uwezo wangu kifedha, hawakujali historia ya familia yangu katika siasa, hawakujali kila mapungufu ambayo nilikuwa nayo, lakini wakaamua kunichagua…..napenda niseme  na kama nilivyosema tangu mwanzo kwamba tumeanza na Mungu na tutamaliza na Mungu na siyo kwenye kupata kura peke yake, tutaendelea kumtumikia Mungu na kumuweka Mungu mbele, tutamtanguliza yeye na tutaongozwa na yeye siku zote”

Haya ni maneno ya mbunge wa CHADEMA mtumishi wa Mungu, Joshua Nasari (26) aliyeshinda Jimbo la Arumeru mashariki kwa kura 32972 ambazo ni sawa na asilimia 54 na kufuatiwa na mgombea wa chama cha mapinduzi, Sioi Sumari aliyepata kura 26,757 sawa na asilimia 42.

Sunday, April 1, 2012

UCHAGUZI ARUMERU MASHARIKI

NASARI JOSHUA
     Ni kitimtim arumeru mashariki, ni kivumbi cha uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo hili kwa sababu kuna mvutano mkubwa kati ya CCM chama cha mapinduzi na CHDEMA chama cha demokrasia na maendeleo. kwa matokeo inaonyesha kuwa chama cha mapinduzi kipo chini kulingana na matokeo ya vituo mbalimbali katika jimbo hili la arumeru mashariki hivyo bas chama cha demokrasia na maendeleo kimeonekana kikiongoza katika maeneo mengi ya hapa arumeru mashariki kikiwemo kituo kilichopo katikati ambacho ni usa river. kwa hali hii sina budi kusema kwamba chama cha demokrasia na maendeleo kimeshika kasi na huenda kikawa kidedea na kushika hatamu hii ya uchaguzi mdogo wa arumeru mashariki.


SIOI SUMARI
     nai jambo la kumshukuru mungu kwani uchaguzi umeenda bila vurugu kubwa kama zile zilizo pita katika uchaguzi uliopita. vurugu zimetokea lakin ni kwa kiasi kidogo sana. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI ARUMERU MASHARIKI.