Monday, May 21, 2012

HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

  TANZANIA MAJONZI KILA KUKICHA
KATIKA BURUDANI

 Ni masikitiko makubwa sana kwa tanzania kuondokewa na watu maarufu na majembe ambao walikua wakitegemewa na familia zao na taifa kwa ujumla ili waweze kuinua uchumi wa tanzani. kwa sasa nchi ambayo ndio inaanza kupata maendeleo kupotelewa na watu ambao walikua ni chachu ya maendeleo ni pigo kubwa sana.

  hajapita miezi mingi Tanzania tuliondokewa na mtu muhimu msanii mkongwe wa muziki aliekua akivutia sana watalii na watu ndani ya nchi aliekua akianza kujijenga na kupanda chati kwa kasi sana kwa staili yake aliokua akiitumia ulale pema mr Ebo. ni msanii aliekua mcheshi na muelewa kwa kila jambo alilokua akiambiwa....

  haijapita miezi kadhaa tena tukaondokewa na nguli wa filamu tanzania charles kanumba. tutakukumbuka sana kanumba kwa filamu zako zilizokua zinauza sana ndani na nje ya nchi.....









KATIKA MICHEZO
Pia hatujakaa muda mrefu patrick mutesa mafisango katutoka kiungo wa simba sports club ale tegemewa na timu pia mashabiki wa simba katika kuinua simba mpaka kileleni tutakukumbuka patrick na tanahitaji na tutahitaji watu kama wewe ni pengo kubwa uliacha tanzania na tanzania simba sports club.....









                                                                                                                                                               TANZANIA nchi yenye amani na utulivu lakini ni nchi ambayo majonzi hayakauki machoni hatujawasahau kina john mjema,steve 2k,na viongo wa serikali kama kina nyerere,omari ali juma, na wegine wengi tutawakumbuka..... tuombe tanzania iwe tanzania yenye amani na furaha sio majonzi kila kukicha